
jumuiya ya wazazi mkoani Morogoro
UTANGULIZI
Umoja wa Wazazi wa CCM uliundwa mwaka 1955 ikiwa ni mwaka mmoja tuu tangu kuundwa kwa Chama cha TANU mwaka 1954. Umoja huu uliundwa ukiwa na misingi mikuu miwili, Elimu pamoja na Malezi. Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wazazi.MAJUKUMU YA JUMUIYA YA WAZAZI.
• Kuhamasisha wazazi na Watanzania wa Rika zote juu ya umuhimu wa Elimu pamoja na kuanzisha na kusimamia shule za Jumuiya.• Kusimamia Maadili na Malezi bora kwa Vijana na Jamii kwa ujumla ili kujenga Taifa lenye maadili na linalosimamia misingi ya utamaduni wa Kitanzania.
• Kusimamia Rasilimali pamoja na shughuli za kiuchumi zilizopo, na kubuni miradi mipya, kwa manufaa ya Jumuiya na Taifa kwa Ujumla.
DIRA
Kuwa Jumuiya ya mfano kwa kuhakikisha inatekeleza majukumu ya Jumuiya kwa ufanisi na Uadilifu na kuhakikisha misingi na maadili ya Chama inasimamiwa kikamilifu kwa ustawi wa Jumuiya na Chama cha CCM kwa ujumla.DHIMA
Kuhakikisha kuwa malengo ya Jumuiya na Chama cha Mapinduzi katika kuboresha maisha ya Watanzania yanafanikiwa kwa kusimamia kazi za Jumuiya, Sera na Ilani za CCM kwa ufanisi, Uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.MALENGO
Kuhakikisha kuwa Wazazi kama nguzo ya jamii wanashiriki katika ustawi wa Chama na Taifa kwa kusimamia Elimu, Malezi na Maadili kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinakua imara na madhubuti siku zote.MIRADI YA JUMUIYA
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro inazo shule mbili za sekondari ambazo ni Mkono wa Mara iliyoko Wilayani Kilosa, iliyoanzishwa mnamo mwaka 1979 na Shule ya sekondari ya mabogo iliyoko katika Wilaya ya Mvomero iliyoanzishwa mnamo mwaka 2000. Uongozi mpya wa Jumuia ya Wazazi Mkoani Morogoro uliochaguliwa mwezi Octoba Mwaka 2012 umejipanga kutekeleza majukumu ya Jumuiya ikiwemo kusimamia kwa ufanisi uendeshaji wa shule zilizo chini ya Jumuiya hiyo na kuziboresha ili ziweze kuwa endelevu na kutoa huduma zinazostahili kwa watoto wetu. Vile vile Uongozi umejipanga kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.CHANGAMOTO ZILIZOPO
• Uhaba wa vitendea kazi (vitabu, madawa, madarasa, nyumba za walimu, mabweni ya wasichana na wavulana na walimu wenye sifa) katika shule zetu zilizopo.• Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule zilizopo pamoja na uanzishaji wa miradi mipya.
• Wazazi kutolipa ada/Karo za watoto zao kwa wakati.
• Gharama kubwa za uendeshaji katika shule zetu ikilinganishwa na mapato yanayopatikana.
• Upatikanaji wa Hati Miliki katika maeneo yanayomilikiwa na J/Wazazi Mkoa wa Morogoro.
• Madeni mbalimbali ya shule ambayo ni malimbikizo ya mishahara, chakula, NSSF na TRA
• Uchafuzi wa Mazingira unaofanywa na wananchi wachache ambao si waungwana (uchomaji misitu, ukataji miti ovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji) katika Milima ya Uluguru.
MIKAKATI ILIYOPO
Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Morogoro imejiwekea vipaumbele sita ambavyo ambavyo imejuipanga kuvitekeleza katika kipindi cha miaka mitano (2012-2017.• Kuimarisha Jumuiya ya Wazazi Morogoro ikiwa ni pamoja na Kuongeza wanachama kwa wingi na kuhakiki wanachama waliopo waweze kulipa ada zao kwa wakati.
• Kukarabati na Kuboresha shule za Sekondari ya Mkono wa Mara iliyopo Kilosa na Mabogo Sekondari iliyopo katika Wilaya ya Mvomero.
• Kujenga Ukumbi na Ofisi ya Wazazi Mkoa katika Wilaya ya Morogoro Mjini.
• Kujenga Kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Wilaya ya Ulanga.
• Kuandaa mashindano mbalimbali kwa lengo la kukuza michezo kwa vijana wetu kwa kuanzisha Wazazi cup, Wazazi Band, na mbio za riadha.
• Kuiboresha Wazazi Saccos ili iweze kuwa endelevu na kuwa na wanachama wengi zaidi ya sasa.
“Jumuiya imara ni ile ambayo viungo vyake vimekamilika na kufanya kazi vizuri. Jumuiya Ni wanachama, Jumuiya Ni Viongozi, Jumuiya Ni Vikao vya utendaji Na utekelezaji, Jumuiya Ni watendaji, Jumuiya ni mali na rasilimali za Jumuiya. Kukamilika kwa viungo vyote hivyo na vikafanya kazi ipasavyo ndio uimara wa Jumuiya yetu.” Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete-Mwenyekiti wa CCM Taifa.
JUMUIYA YA WAZAZI MOROGORO
S.L.P 230
Simu/ Nukushi: 023 2613538
Barua Pepe: wazazimoro@gmail.com
Tovuti: www.wazazimorogoro.blogspot.com
Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro,Mh.Mecky Mdaku akiwa katika ziara maalum ya kukimarisha Chama cha Mapinduzi CCMwilayani Gairo,Morogoro
Subscribe to:
Posts (Atom)